Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bilioni 2.3 zahitajika kwenye maeneo ya mizozo ili kupeleka watoto shule:UNESCO

Bilioni 2.3 zahitajika kwenye maeneo ya mizozo ili kupeleka watoto shule:UNESCO

Mada mpya iliyochapishwa katika Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) ya ufuatiliaji wa elimu kwa wote duniani, EFA GMR imesema kuwa dola Milioni Mbili nukta Tatu zahitajika ili kupeleka shule watoto Milioni 34 walioko kwenye maeneo yenye mizozo.

Idadi hiyo ni pamoja na vijana barubaru ambao wamelazimika kutohudhuria shule kutokana na mazingira duni ambapo ripoti inasema kiasi hicho cha fedha ni mara kumi zaidi ya kiwango ambacho sekta ya elimu inapatiwa kupitia msaada wa kibinadamu.

Ripoti hiyo imetupia lawama migogoro inayoendelea duniani ambayo inasababisha wahisani kutochangia sekta ya elimu kwani inajikuta inapata asilimia mbili tu kutoka misaada ya kibinadamu.

Hata hivyo ripoti hiyo inasema kiwango pia kilichopendekezwa hivi sasa ambacho ni asilimia Nne kilichopigiwa chepuo tangu mwaka 2011 hakitoshi.