Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua de Clercq kuwa mwakilishi wake Somalia

Ban amteua de Clercq kuwa mwakilishi wake Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon leo ametangaza uteuzi wa Peter de Clercq wa Uholanzi kuwa msaidizi wa mwakilishi maalum wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOM) ambapo pia atatumikia nafasi ya mratibu mkazi, mratibu wa masuala ya kibinadamu na mwakilishi mkazi wa shirika la UM la mpango wa maendeleo(UNDP).

Taarifa ya mseaji wa Katibu Mkuu inasema kuwa Bwana de Clercq atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Philippe Lazzarini wa Switzerland anayekwenda kufanyakazi katika ofisi ya mratibu maalu wa UM kwa ajilli ya Lebanon (UNSCOL). Katibu Mkuu amemshukuru Bwana Lazzarini kwa uongozi wake nchini Somalia.

Taarifa hiyo imeeleea kuwa mteule Bwana de Clercq ana uzoefu katika masuala ya siasa, usalama, operesheni na dharura, ulinzi wa raia, utawala wa sheria pamoja na utawala wa masuala ya kibinadamu na usaidizi wa maendeleo.

Amefanya kazi kama mwakilishi mkazi na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Sudan pamoja na kufanya kazi kwenye shirika la UM la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa miaka 27.