Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon alaani shambulizi la kanisa la Charleston

Ban Ki-moon alaani shambulizi la kanisa la Charleston

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali mauaji ya watu tisa yaliyotokea tarehe 17 Juni, mjini Charleston, Marekani.

Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa Umoja wa Mataifa inasema kwamba shambulizi hilo lililotokea kwenye kanisa la kihistoria la jamii ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika, linadaiwa kuwa na msingi wa chuki ya ubaguzi wa rangi.

Bwana Ban amepeleka salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga akiwapa pole waliojeruhiwa.

Hatimaye Katibu Mkuu amesema anatumai kwamba yule au wale waliotekeleza uhalifu huo unaochukiza watapelekwa mara moja mbele ya sheria.