Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasaidia familia za wakimbizi waliohamia shule za Benghazi, Libya

UNHCR yasaidia familia za wakimbizi waliohamia shule za Benghazi, Libya

Shirika la kuwahudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, likishirikiana na mashirika ya LibAid na CESVI, limekamilisha usambazaji msaada wa bidhaa zisizo za chakula kwa familia za wakimbizi wa ndani ambao wametafuta hifadhi katika shule za mji wa Benghazi nchini Libya.

Familia nyingi za wakimbizi wapya wa ndani ambao hawana namna nyingine, walilazimika kutafuta makazi katika shule, na wengine kuhamia katika shule hizo jamii za wenyeji wao zinapoishiwa uwezo wa kukidhi mahitaji yao.

UNHCR imesema kuwa familia hizo ambazo zimeathiriwa na mapigano kwenye mji huo kwa miezi kadhaa sasa, zina mahitaji ya kibinadamu ya dharura, na usambazaji huo ulilenga kuwapa ahueni wakimbizi wapya waliokimbilia shule hizo.