Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaendesha mafunzo ya usalama wa wanahabari Somalia

UNESCO yaendesha mafunzo ya usalama wa wanahabari Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) kwa kushirikiana na mamlaka za usalama nchini Somalia limeendesha semina kuhusu wajibu wa vikosi hivyo katika kupatia ulinzi usalama wanahabari ili kukuza demokrasia.

Ikimnukuu waziri wa habari wa utamaduni na utalii wa Somalia UNESCO inasema kuwa semina hiyo iliyofanyika June 2 hadi 4 na kujenga ubia mwema kati ya vikosi vya ulinzi na vyombo vya habari ili kufanikisha Somalia moja yenye demokrasia, amani na thabiti.

Kwa mujibu wa UNESCO mafunzo hayo ambayo yameratibiwa kwa ushirikiano na wizara ya habari, vikosi vya usalama na muungano wa wanahabari nchini Somalia NUJOS, yametoa fursa kwa washiriki kujifunza kwa vitendo kufuatia mifano halisi iliyotolewa na wataalamu wa kimataifa waliojadili jukumu la vyombo vya usalama katika kuhakikisha wanahabari wanapata taarifa.

Mafunzo hayo yalizingatia muongozo wa UNESCO katika uhuru wa kujieleza na mamlaka ya umma ambapo hupatia vikosi vya usalama, nyenzo za nadharia na vitendo katika kutekeleza jukumu lao la kulinda amani ilihali wakizingatia haki za binaadamu, uhuru wa kujieleza na usalama wa wanahabari.