Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoshirikisha wanawake kwenye ujenzi wa amani ni dhihaka: Eliasson

Kutoshirikisha wanawake kwenye ujenzi wa amani ni dhihaka: Eliasson

Nafasi ya wanawake katika kuongoza masuala ya amani na usalama ni lazima yapatiwe kipaumbele awali badala ya kusubiri mwishoni mwa mchakato mzima, amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson alipozungumza jijini New York.

Akihutubia washiriki wa kikao cha kutathmini utekelezaji wa ajenda ya ushiriki wa wanawake kwenye mchakato wa amani na usalama Bwana Eliasson amesema mara nyingi ushiriki wa wanawake unakuwa ni finyu au haupo kabisa akitolea mfano…

(Sauti ya Eliasson)

“Naweze kuwaeleza kwa masikitiko kuwa nilishasuluhisha mizozo kama sita tangu mwanzoni mwa miaka  ya 90 na kamwe sikuwahi kuona mwanamke kwenye upande wa pili wa meza ya mazungumzo. Ni ukosefu wa kutisha katika mchakato mzima wa ujenzi wa amani.”

Amesema ushirikishaji wanawake huzaa matunda na hilo liko dhahiri akigusia vile ambavyo Katibu Mkuu amekuwa akipigia chepuo ushirikishwaji wa wanawake katika ujenzi wa amani baada ya mizozo na ni matarajio yake kuwa..

(Sauti ya Eliasson)

“Tathmini ya ulinzi wa amani unaofanywa na jopo huru la ngazi ya juu na kutarajiwa kukamilika katikati ya mwezi Juni ni lazima ijumuishe kama suala muhimu uwezeshaji wanawake na uongozi katika uzuiaji na usuluhishaji wa mizozo.”