Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utashi wa kutokomeza waasi DRC bado upo:Paluku

Utashi wa kutokomeza waasi DRC bado upo:Paluku

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, Martin Kobler,ameongoza shughuli ya utoaji heshima za mwisho kwa watanzania wawili waliouawa kwenye mashambulizi, maeneo ya Beni, tarehe 7 mwezi huu.

Bwana Kobler amesema walinda amani hao wawili, John Leonard Mkude na Juma Ali Khamis, wameuawa wakitetea  amani nchini DRC

Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Julien Paluku alishiriki tukio hilo akisema..

“  Wakati huu tunataka kukariri kwa niaba ya serikali kwamba utashi ni mkubwa ili kutokomeza waasi wanaosambaa kwenye eneo hilo. Licha ya matukio hayo, najua kwamba utashi wa Umoja wa Mataifa na serikali bado ni kuhakikisha kwamba nchi hii irejeshwe amani,  heshima na utu wake.”