Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yatiwa hofu na kuongezeka mvutano baina ya kabila la Rezeigat na Ma’alia Mashariki mwa Darfur

UNAMID yatiwa hofu na kuongezeka mvutano baina ya kabila la Rezeigat na Ma’alia Mashariki mwa Darfur

Vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur UNAMID vimesema vinatiwa hofu na kuongezeka kwa mvutano baina ya kabila la Rezeigat na Ma’alia Mashariki mwa Darfur nchini Sudan..

UNAMID imezichagiza pande hizo mbili kujizuia na machafuko na kujihusisha katika majadiliano ili kutatua mzozo uliopo badala ya kutumia nguvu na vitendo vya ghasia zvitakavyosababisha madhila zaidi.

Mpango huo wa kulinda amani umekaribisha hatua ya serikali ya Sudan kuongeza vikosi ili kuunda eneo la usalama lililozuiliwa baina ya makabila hayo mawili na pia kuendelea na juhudi za kudhibiti mvutano. UNAMID imetoa wito kwa serikali ya Sudan kuongeza juhudi zake kuhakikisha mvutano huo hausababishi kuzuka kwa vita.