Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaomba uchunguze ufanyike juu ya mauaji ya wahamiaji baharini

IOM yaomba uchunguze ufanyike juu ya mauaji ya wahamiaji baharini

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM leo limeomba uchunguzi ufanyike kwa ngazi ya kimataifa kuhusu maangamizi ya meli baharini, baada ya meli moja iliyozama kupatikana alhamis ikidaiwa na mabaki ya mamia ya watu.

Msemaji wa IOM Joel Millman amewaambia waandishi wa habari kwamba mamlaka za serikali ya Italia zilifanya ugunduzi wa maangamizi hayo kwa kutumia roboti.

Kwa mujibu wa wahamiaji 28 waliookoka wakati meli ilipozama, meli hiyo ilikuwa na abiria takriban 800.

Katika taarifa iliyotolewa leo, IOM imepongeza juhudi za Italia za kupeleka wasafirishaji haramu mbele ya sheria, ikiomba uchunguzi ufanyike kuhusu tukio hilo, ikisema kwamba ni uhalifu wa hali ya juu.

Aidha IOM imeshangazwa na kuongezeka kwa idadi ya vifo baharini, iliyofika 1,829 tangu mwanzo wa mwaka ikilinganishwa na 207 mwaka jana.

Mwaka huu idadi kubwa ya wahamiaji wanatoka Eritrea, halikadhalika Somalia, Nigeria, Gambia na Syria.