Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 100,000 wapoteza makazi yao jimbo la Unity pekee: OCHA

Watu 100,000 wapoteza makazi yao jimbo la Unity pekee: OCHA

Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA imesema operesheni za kijeshi kusini mwa Bentiu, mji mkuu wa jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, zimesababisha watu Laki Moja kukimbia makazi yao tangu mwanzoni mwa mwezi huu pekee.

Mratibu wa ofisi hiyo nchini Sudan Kusini, Toby Lanzer Lanzer amenukuliwa akisema wakazi wa maeneo ya Guit, Ngop na Nhialdu waliokuwa wamenaswa kwenye mapigano, hatimaye wameweza kukimbia na hali hiyo ambayo si nzuri imekuja wakati huu ambao ni msimu wa upanzi na wananchi wanatakiwa wawe huru waweze kupanda mazao.

Mratibu huyo amesema wanachofanya sasa na wadau wao ni kusaka mbinu za kuwafikia wananchi hao ili waweze kufanya tathmini ya mahitaji huku wakisihi pande husika kwenye operesheni hizo kulinda raia kwa mujibu wa sheria za kibinadamu za kimataifa.