Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huku vifo vitokanavyo na ukatili vikipungua mizozo inakuwa hatari zaidi:UNDP

Huku vifo vitokanavyo na ukatili vikipungua mizozo inakuwa hatari zaidi:UNDP

Zaidi ya watu bilioni 1.5 kote duniani wanaishi katika maeneo ambako kunashuhudiwa ukatili na mzozo ambako kuna changamoto ya silaha ndogo ndogo na ukatili zaidi na uhasama mkubwa kati ya makundi mbali mbali. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Hiyo ni kauli ya Neil Buhne Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango ya Maendelo la Umoja wa Mataifa UNDP, mjini Geneva wakati wa uzinduzi wa ripoti iitwayo Mzigo wa dunia wa ukatili wa silaha 2015:Kila mtu ana umuhimu.

Ripoti inakadiria takriban vifo zaidi ya Laki Tano  vilitokea kila mwaka kati ya 2007 hadi 2012 ikiwa imepungua ikilinganishwa na 2011, idadi kubwa ikiwa ni matokeo ya moja kwa moja ya mzozo.

Ripoti hiyo inasema kwamba wakati hali ya kupungua kwa vifo kutokana na ukatili ikishuhudiwa, athari za kiuchumi ni dhahiri kulingana na Anna Alvazzi del Frate ambaye ni mkuu wa utafiti wa silaha ndogo ndogo..

Mwaka wa 2010 dola biloni 171 gharama ya maafa kutokana ukatili usio husiana na mizozo. Idadi hiyo imepanda ikilinganishwa na bilioni 160 mwaka 2000. Inaripotiwa kuwa kadri nchi inavyoendelea, gharama nayo inazidi. Lakini hii haimaanishia kuwa ghasia ina madhara madogo kwa nchi zinazoendelea.”

Hata hivyo pendekezo ni kuzuia ukatili ili kupunguza gharama ya ukatili.