Tuchukue hatua tuokoe jamii dhidi ya madawa ya kulevya: Kutesa

7 Mei 2015

Kuelekea kikao maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani hapo mwakani, hii leo baraza hilo limekuwa na mjadala wa ngazi ya juu ukiwa na lengo la kuunga mkono mchakato huo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Hakuna nchi ambayo iko salama kutokana na janga la madawa ya kulevya na madhara yake kwa jamii, amesema Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa alipofungua kikao hicho. Amesema biashara hiyo haramu ina thamani ya mabilioni ya dola ilhali wakulima wake ni hohehahe, hivyo..

(Sauti ya Kutesa)

“Watu lazima wawe kitovu cha juhudi zetu zote na tufanye tuwezalo ili tuwaepushe na mazingira yanayowatumbukiza kwenye madawa ya kulevya na uhalifu.”

Jan Eliasson, Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akaangazia suluhisho..

(Sauti ya Eliasson)

“Tiba dhidi ya utegemezi wa madawa, kuwapatia huduma ya afya na hifadhi ya jamii na kusaidia mbinu halali mbadala za kuishi ni mambo muhimu katika kudhibiti madawa ya kulevya.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter