Skip to main content

FAO yatabiri kupungua kwa bei za uagizaji wa vyakula kutoka nje.

FAO yatabiri kupungua kwa bei za uagizaji wa vyakula kutoka nje.

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema uagizaji wa vyakula kutoka nje umeendelea kupungua na unatarajiwa kuvunja rekodi mwaka huu wa 2015.

Ripoti ya mtazamo kuhusu chakula ikiangazia vipimo vya bei na uagizaji ambayo imechapishwa leo imesema kupungua kumechochewa na sababu kadhaa ikiwemo kuimarika kwa sarafu ya Marekani, dola na kuwepo kwa akiba kubwa ya chakula sambamba na kuendelea kushika kasi kwa sekta ya uvuvi.

Abdolreza Abbassian ni mchumi mwandamizi wa FAO.

(Sauti ya Abbassian)

"Kwa ujumla hali hii ya upatikanaji  mkubwa wa bidhaa umeathiri bei hususan kupungua kwa bei kunakoshuhudiwa na  huenda ikawa ni sababu ya kupungua kwa uagizaji bidhaa kutoka nje."

Kwa mujibu wa FAO uzalishaji nafaka unaweza kupungua kwa asilimia 1.5 ikilinganishwa na mwaka jana lakini hali hiyo haitakuwa na athari kutokana na uwepo wa akiba za vyakula na nchi za vipato vya chini zinatarajiwa kunufaika na mwelekeo huo.