Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kwa watoto takriban milioni 1 Nepal iko mashakani:UNICEF

Elimu kwa watoto takriban milioni 1 Nepal iko mashakani:UNICEF

Takriban watoto 95,000 nchini Nepal hawataweza kurejea shuleni isipokuwa tu kama hatua itachukuliwa haraka kutoa maeneo ya muda ya kusomea na kukarabati majengo ya shule yaliyoharibiwa vibaya wakati wa tetemeko la ardhi la April 25 limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Madarasa yapatayo 24,000 yalibomolewa au kusambaratishwa kabisa na tetemeko hilo. Kiwango cha tatizo la elimu kinatarajiwa kuongezeka katika siku na wiki zijazo kutokana kupatikana kwa taarifa ziadi kutoka maeneo ya vijijini. Shele zinatarajiwa kufunguliwa Mai 15.

Watoto karibu milioni moja walioandikishwa shule kabla ya tetemeko huenda sasa wakabaini hawana shule ya kwenda amesema Tomoo Hozumi mwakilishi wa UNICEF nchini Nepal.

UNICEF inahofia kwamba hatua kubwa iliyopigwa nchini humo kwa miaka 25 iliyopita katika kuongeza uandikishaji wa watoto katika elimu ya msingi kutoka asilimi 64 mwaka 1990 hadi kufikia Zaidi ya asilimi 95 hii leo , inaweza kupata pigo kufuatia athari za tetemeko.