Skip to main content

Zaidi ya wakimbizi 4000 wa Burundi waingia Tanzania

Zaidi ya wakimbizi 4000 wa Burundi waingia Tanzania

Nchini Burundi hali si shwari na raia wake wameendelea kukimbilia nchi jirani na ripoti za hivi karibuni zaidi zinasema wameingia Tanzania kwa hofu ya sintofahamu iliyoibuka nchini mwao. Taarifa ya Amina Hassan inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Amina)

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unasema idadi kubwa ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto na kasi ya kuingia nchini humo inaongezeka kila uchao. Mwakilishi mkazi wa Umoja huo nchini Tanzania Alvaro Rodriguez anasema kile ambacho wanafanya hivi sasa.

(Sauti ya Alvaro)

Bwana Alvaro amesema kwa sasa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linashauriana na wahisani ili kuongeza usaidizi wa huduma za msingi kwa wakimbizi hao ikiwemo chanjo wakati huu ambapo serikali ya Tanzania imeshajadili suala la kutoa eneo la kujenga kambi nyingine iwapo idadi itaongezeka zaidi.