Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO, EBRD na UFM kuimarisha usalama wa chakula ukanda wa Mediterranean:

FAO, EBRD na UFM kuimarisha usalama wa chakula ukanda wa Mediterranean:

Kuinua uzalishaji wa kilimo endelevu na biashara ni moja ya masuala yanayopewa kipaumbele katika maeneo ya Kusini na Mashariki mwa ukanda wa Mediterranean, ambako nchi nyingi zinazalisha idadi ya chakula isiyotosheleza.

Na kwa sababu hiyo shirika la chakula na kilimo (FAO), Benki ya Ulaya kwa ajili ya ujenzi na maendeleo (EBRD) na muungano wa Mediteraniani (UFM) wameandaa kongamano la usalama wa chakula Kusini na Mashariki mwa Ukanda wa Mediteraniani.

Kongamano hilo la siku mbili (Mai 5-6) ni la kuboresha ushirikiano baina ya sekta za umma na binafsi , kuanzisha wakulima na mashirika yao hadi makampuni madogo, ya kati na makubwa ya biashara na kilimo, na kuanzisha mpango wa kuongeza uwekezaji katika kilimo na mifumo ya chakula.

Kongamano hilo limewaleta pamoja watunga sera wa ngazi ya juu, taasisi za fedha na wawakilishi kutoka sekta binafsi, vituo vya utafiti na wanazuoni.

Kongamano linatoa fursa ya kujadili jinsi gani sekta za umma na binafsi zinaweza kushirikiana kuinua usalama wa chakula katika ukanda huo kwa kuwezesha uwekezaji endelevu unaokwenda sambamba na ukuaji wa idadi ya watu.