Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO/UNHCR watoa muongozo mpya kuhusu afya ya akili kwenye majanga ya kibinadamu:

WHO/UNHCR watoa muongozo mpya kuhusu afya ya akili kwenye majanga ya kibinadamu:

Duniani kote takribani watu milioni 80 hivi sasa wanaathirika na dharura za kibinadamu kuanzia majanga ya asili na vita vya silaha kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Sudan Kusini, Syria, Yemen na kwingineko ikiwemo tetemeko la karibuni la Nepal.

Shirika la afya duniani WHO linakadiria kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu wanaosumbuliwa na afya ya akili kama msongo wa mawazo ni matokeo ya dharura za kibinadamu.

Limeongeza kuwa watu wenye maradhi ya afya ya akili mara chache sana wanapata fursa ya wataalamu wa afya wa kutathimini na kukabiliana na hali yao.

Kwa pamoja WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wametoa muuongozo mpya ujulikanao kama ” Muongozo wa hatua za kibinadamu katika kuziba pengo la afya ya akili”(mhGAP-HIG) ambao utahakikisha wafanyakazi wasio wataalamu wa afya hawashughulikia kubaini, kutathimini na kushughulikia mahitaji ya afya ya akili.

Pia muungozo huo unaeleza kwa vitendo, usimamizi wa mapendekezo ya afya ya akili, mishipa ya fahamu na hali ya matumizi madawa.