Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji hatuthaminiwi: Watu wa asili

Wafugaji hatuthaminiwi: Watu wa asili

Mwakilishi wa jamii ya asili ya wafugaji iitwayo Samburu kutoka Kenya ambaye pia anawakilishja mfuko wa wanawake wa jamii hiyo, Samburu Women Trust, Jane Meriwas amesema ni muhimu jamii ya kimataifa na kitaifa itambue haki za wafugaji na kuipa fursa jamii hiyo ambayo inaishi kwa kuhamahama kutokana na kutafuta malisho.

Katika mahojiano na idhaa hii mjini New York anakohudhuria kongamano la 14 la watu wa asili Bi Meriwasi amesema jamii za wafugaji nchini Kenya zimeathiriwa na mambo mengi ikiwamo mabadiliko ya tabianchi.

(SAUTI JANE)

Hata hivyo amesema licha ya kwamba sera ya nchi haitoi kipaumbele kwa jamii ya wafugaji lakini taasisi yake inajitahidi kuwawezesha wanawake.

(SAUTI JANE)