Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunawawezesha vijana kiuchumi : Kijana Robert

Tunawawezesha vijana kiuchumi : Kijana Robert

Mwakilishi wa asasi ya kiraia kutoka Kenya iitwayo mtandao wa barubaru na vijana Afrika, NAYA kwa upande wa Kenya Robert Aseda amesema kabla ya kusubiri uwezeshaji kutoka nje shirika hilo linatumia ujuzi wa vijana mbalimbali kwa kuwaimarisha.

Robert Aseda ambaye ni Afisa Mradi wa NAYA alikuwa ni miongoni mwa vijana kutoka Afrika waliohudhuria mkutano wa 14 wa kamisheni ya maendeleo na idadi ya watu CDP ulimalizika mwishoni mwa wiki mjini New York. Aseda amefanya mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii muda mchache kabla ya kulekea Kenya na anaanza kueleza ujumbe wa asasi yake katika mkutano huo.

(SAUTI MAHOJIANO)