Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya tumbaku yanapungua, lakini vita bado- WHO

Matumizi ya tumbaku yanapungua, lakini vita bado- WHO

Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO, zinaonyesha kupungua kwa matumizi ya tumbaku na kuongezeka idadi ya watu wasiovuta sigara. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Taarifa ya Joshua)

WHO imesema licha ya mwelekeo huo, serikali zinapaswa kuongeza juhudi za kupambana na sekta ya tumbaku na kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya bidhaa za tumbaku ili kulinda afya ya umma.

Kutovuta sigara sasa kunakuwa jambo la kawaida kote duniani, kwa mujibu wa ripoti hiyo kuhusu mwelekeo wa matumizi ya tumbaku duniani, ambayo imezinduliwa leo mjini Abu Dhabi wakati wa kongamano la 16 kuhusu Tumbaku au Afya.

Kongamano hilo linalohitimishwa mnamo Machi 21, linamulika udhibiti wa tumbaku na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs), mathalan yale ya mapafu na moyo, saratani na kisukari.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mnamo mwaka 2010, kulikuwa na watu bilioni 3.9 juu ya umri wa miaka 15 wasiovuta sigara, ambayo ni asilimia 78 ya idadi ya watu bilioni 5.1 wenye umri huo.