Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga ya asili huzorotesha maendeleo: Benki ya dunia

Majanga ya asili huzorotesha maendeleo: Benki ya dunia

Kuendelea kukuwa kwa majanga ya asili kote duniani kunarudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa mujibu wa benki ya dunia.

Kwa mujibu wa benki ya dunia madhara ya majanga ya asili kwa pato la nchi (GDP) ni mara 20 zaidi kwa nchi zinazoendelea ikilinganishwa na zile zenye viwanda.

Rachel Kyte, ni mjumbe maalum wa benki ya dunia kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi na ni miongoni mwa mamia ya wahudhuriaji wa kongamnao kuhusu kupunguza majanga ambalo limemalizika mjini Sendai Japan.

Nan zheng wa redio ya Umoja wa Mataifa amemuuliza namna kupunguza majanga kunavyoweza kusaidia ajenda ya benki ya dunia ya kusaidia mandeleo ya kiuchumi ya nchi

(SAUTI RACHEL)

"Changamoto kubwa ni kupata maendeleo yanayoweza kukabiliana na majanga, la pili ni kubadilisha mfumo wa matumizi ya fedha hasa pale tunapotumia fedha nyingi katika misada ya kibinadamu, ukwamuaji namakabiliano na sio kinga. Changamoto ya tatu ni kufahamu nini huwazuia watu kuchukua hatu hata kama wana taarifa na ujuzi."