Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumuishaji wa walemavu hujenga uthabiti dhidi ya majanga

Ujumuishaji wa walemavu hujenga uthabiti dhidi ya majanga

Ujumuishaji ndiyo njia bora zaidi ya kujenga uthabiti. Huo ndio ujumbe walioupeleka watu wenye ulemavu kwenye kongamani la tatu la kimataifa kuhusu kupunguza hatari za majanga, ambalo limehitimishwa mjini Sendai, Japan.

Kongamano hilo limeelezwa kuwa hatua zimepigwa kwa kiasi kikubwa, lakini juhudi zaidi zinahitajika kuhusu ujumuishaji na kuweka mifumo inayowawezesha watu wenye ulemavu kupata chochote, kuanzia miundo mbinu hadi matangazo ya kutoa tahadhari za mapema.

Wajumbe kwenye kongamano hilo wamekumbushwa kuwa udhibiti wa hatari za majanga unaojumuisha kila mtu, wakiwemo watu wenye ulemavu, ni njia moja ya kuchangia uendelevu.

Zaidi ya asilimia 15 ya idadi nzima ya watu duniani, ikiwa ni takriban watu bilioni moja, wanaishi na ulemavu. Watu wenye ulemavu hukumbwa na hatari kubwa zaidi na huathiriwa zaidi na majanga, hali za dharura na mizozo, wakilinganishwa na watu wengine kwa ujumla.