Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viashiria viende sambamba na malengo endelevu: Tanzania

Viashiria viende sambamba na malengo endelevu: Tanzania

Mkutano wa 46 wa kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa unaendelea kwenye makao makuu ya Umoja huo ambapo moja ya masuala yanayojadiliwa ni jinsi ya kuweka viashiria vitakavyojumuishwe kwenye malengo ya maendeleo endelevu yanayotarajiwa kupitishwa na wakuu wa nchi mwezi Septemba mwaka huu.

Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo, Dkt. Albina Chuwa ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ameiambia Idhaa hii kuwa hoja kubwa iliyopo ni kujumuisha viashiria vya utekelezaji kama vile vya umaskini na afya kwenye malengo hayo badala ya kusubiri.

(Sauti ya Dkt. Chuwa)