Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlo mashuleni ni muhimu kwa mustakhbali wa mtoto: WFP

Mlo mashuleni ni muhimu kwa mustakhbali wa mtoto: WFP

Mlo mashuleni ni muhimu kwa mustakhbali wa mtoto limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo hugawa chakula mashuleni kwa maelfu ya watoto.

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya mlo mashuleni WFP inasema utoaji wa mlo mashuleni unasaidia kupambana na utapia mlo ambao unawakabili watoto wengi walio chekechea na shule za msingi, lakini pia ni uwekezaji mzuri wa mustakhbali wa maisha ya watoto.

WFP ina mradi wa mlo mashuleni katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Lesotho ambako watoto 250, 000 wa cheklechea na shule za msingi wamefaidika mwaka 2014 huku wengine 190,000 wanapatiwa milo miwili kwa siku kupitia mradi unaoongozwa na serikali kwa msaada wa WFO utakaoendelea hadi 2018.

Kwa mujibu wa WFP mradi wa mlo mashuleni una lengo la kukabiliana na matatizo ya ukosefu wa lishe, kuchagiza maeendeleo ya watoto shuleni na kuwahimiza wazazi kuwaingiza watoto chekechea hadi watakapofikia umri wa kuanza shuke la msingi.