Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za chakula zimeshuka zaidi mwezi Februari zikiongozwa na sukari:FAO

Bei za chakula zimeshuka zaidi mwezi Februari zikiongozwa na sukari:FAO

Shirika la Chakula na Kilimo(FAO) limesema bei za chakula zimeshuka tena kwa asilimia 1 mwezi wa Februari ikilinganishwa na Januari na zimeporomoka kwa asilimia 14 ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana.

Bei zilizoporomoka ni za nafaka, nyama na hasa sukari huku bei za maziwa na mafuta ya chikichi zikiongezeka kidogo. Kwa mujibu wa FAO kushuku huku kunakoendelea ni kwa kiwango cha chini sana tangu Julai mwaka 2010 na kumechangiwa na mazingira ya usambazaji wa chakula pamoja na kushuka kwa sarafu za nchi nyingi dhidi ya dola za Kimarekani .

Hata hivyo mtaalamu wa soko la maziwa na mifugo wa FAO Michael Griffin anasema, kitu cha muhimu ni mtazamo wa uzalishaji kwa mwaka 2015 unaotia matumaini na akiba nzuri ya nafaka iliyopo.