Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake, wasichana kuwezeshwa kielimu kupitia simu za mikononi

Wanawake, wasichana kuwezeshwa kielimu kupitia simu za mikononi

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikina na shirika la masuala ya wanawake katika Umoja wa Mataifa UN WOMEN wameandaa juma la mafunzo kwa njia ya simu za mkononi kwa 2015 ( MLW 2015).

Kwa mujibu wa UNESCO wiki hiyo ya mafunzo kwa nji ya simu za mkononi yatakatyofanyika tareje 23 hadi 27 mwezi Februari yataangazia namna teknolojia ya simu za mikononi inavyoweza kusukuma mbele kiwango bora cha elimu kwa wanawake na wasichana hususani wale wanaoishi katika jamii ambazo hazijafikiwa.

UNESCO inasema maudhui haya ya teknolojia ya simu za mikononi na maendeleo ya elimu kwa wanawake na watoto yanapewa umuhimu na fursa sawa, mukatdha wa usawa wa kijinisia na ufundisahaji, kujua kusoma na kuandiak na maendeleo ya ujuzi.

Wiki ya mafunzo kwa nji aya simu za mikononi mwaka huu (MLW 2015), itagawanywa katika njia tofauti ili kupanua wigo wa ushiriki ambapo watunga sera, mameneja wa miradi, wawezeshaji kitaaluma na wafanya utafiti watahusishwa.