Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapongeza juhudi za kuridhia mkataba wa usafiri wa kwenye maji

Picha:IMO

IOM yapongeza juhudi za kuridhia mkataba wa usafiri wa kwenye maji

Katika Mkuu wa Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM Koji Sekimizu amekaribisha nafasi iliyochukuliwa na Shirika la Meli la kimataifa ambalo limechukua hatua muhimu kuwezesha kuridhiwa kwa mkataba wa kimataifa wa kuhifadhi na kudhibiti usafiri wa maji.

Katika taarifa yake katibu huyo amesema kuwa hatua ya shirika hilo kuweka mikakati kuhusiana na mkataba huo itatoa msukumo kwa nchi ambazo bado haijaridhia mkataba huo na kwamba nchi hizo sasa zinaweza kuharakisha zoezi la uridhiaji.

Akizungumza mara baada ya kukutana na mkuu wa shirika hilo la meli za kimataifa, Koji amesema kuwa ni matumaini yake nchi husika zitachukua hatua za haraka kuridhia mkataba huo na kwamba zitafanya hivyo pia kwa kuzingatia masharti yaliyomo.