Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yawapiga jeki vijana Zambia

Innocent Makumbalaying ni mwanafunzi wa shule ambayo inashiriki na mradi BEAR nchini Zambia. Picha: UNESCO

UNESCO yawapiga jeki vijana Zambia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO katika mpango wake wa Elimu ya Msingi kwa ajili ya ustawi wa  Afrika (BEAR) linawasaadia  wanafunzi kujifunza taaluma mbali mbali mathalan, useremala, utengenezaji wa umeme na kurekebisha mabomba.  Mpango huo unatekelezwa katika mataifa matano ya Afrika, ikiwamo Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Malawi, Namibia na Zambia. Taarifa kamili na Geroge Njogopa.

(Taarifa ya George)

Innocent Makumba mwenye umri wa miaka 38 ni miongoni mwa vijana hao walidhamiria kupata elimu ya ufundi na tayari wameanza kuonyesha uwezo wao.

Yeye na vijana wengine 5o wanapata mafunzo ya ufundi staadi kwenye shule hiyo ambayo imebuniwa na UNESCO kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana.

Wakiwa shuleni hapo vijana hao watajifunza kazi za utengenezaji matofali, ufundi umeme, na ujenzi wa kawaida na kwamba wako tayari kuunga mkono juhudi za UNESCO kuijenga vyema shule hiyo iliyoko Kusini mwa Zambia.