Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima juhudi ziongezwe kutokomeza Ebola; Ban

UN Photo/Martine Perret
Picha:

Lazima juhudi ziongezwe kutokomeza Ebola; Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye amehitimisha ziara yake ya kutathimini hali ya ugonjwa wa homa kali ya Ebola katika nchi zilizoathiriwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi amesema licha ya hatua kadhaa zilizochukuliwa bado kuna mengi ya kufanya . Taarifa zaidi na Abdullahi Boru.

(TAARIFA YA ABDULLAHI)

Katibu Mkuu amesema  nchi zilizoathiriwa na Ebola zimefanya  juhudi kubwa katika kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo lakini akasema hatua nne za dharura zinazopaswa kuchukuliwa sasa ni

( SAUTI ya Ban)

"Kwanza tunarekebisha mfumo ili uende sawa na taswira ya janga. Tunashuhudia kuwa mlipuko unakuwa na hivyo kuathiri maeneo mengi. Kwahiyo lazima tuchukue hatua."

Bwana Ban amesema hatua ya pili ni kuongeza juhudi katika kutokomeza maambukizi hadi mashinani na tatu ni ujenzi mpya wa kijamii , kielmuna hata kiuchumi kw anchi zilizoathiriwa.

Kadhalika Katibu Mkuu amesema hatua ya mwisho ya nne ya kuchukuliwa ni somo kw ajumuiya ya kimataifa kujifunza somo na kuchukua tahadhari kuhusu Ebola na majanga mengine.