Ujumbe wa umoja wa Mataifa Burundi wafunga wakati wa maandalizi ya uchaguzi
Nchini Burundi, ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa (BNUB) unatakiwa kufunga ofizi zake rasmi mwisho wa mwezi huu, tarehe 31, Disemba.
Hii inafuataia uamuzi wa serikali ya nchi hiyo ikiwa ni miaka 10 tangu BNUB ifunguliwe nchini humo.
Wakati huo huo, serikali ya Burundi inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Machi mwaka kesho na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo umeshirikiana katika maandalizi ya uchaguzi huo na mazungumzo ya kisiasa.
Licha ya upinzani na jamii kulaani kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu na kuhofia migogoro wakati wa uchaguzi, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi umekaribisha hatua zilizofikiwa katika kuboresha mazungumzo ya kisiasa.
Vladimir Monteiro ni msemaji wa BNUB
«Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na mzozo uliofuata, hakukuwa tena na mazungumzo baina ya serikali na upinzani. Vitu vingi vimebadilika, kumekuwa mazungumzo kuhusu sheria ya uchaguzi. Kanuni za maadili zimekubaliwa baina ya serikali, chama tawala na vyama vya upinzani. Baadhi ya sheria zinazozuia uhuru wa watu zinaweza kuathiri utaratibu wa uchaguzi, tunajua hilo. Ndio maana tunasitawisha mazungumzo hayo ili uchaguzi utekelezwe vizuri bila migogoro”