Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya ugaidi dhidi ya raia vyamchukiza Ban

UN Photo/Albert Gonzalez Farran
Picha:

Vitendo vya ugaidi dhidi ya raia vyamchukiza Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kufedheheshwa kwa mashambulizi dhidi ya raia ambapo amelaani vitendo hivyo vinavyolenga wananchi wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Ban akitolea mfano mashambulizi ya wiki hii pekee huko Nigeria, Yemen na Pakistan akitaka wahusika wa vitendo hivyo wafikishwe mbele ya sheria.

Aidha, Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na kuonyesha mshikamano wake na serikali na watu wa nchi husika katika vita dhidi ya ugaidi.