Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Imani ya wananchi kwa UM ni muhimu ili kufanikisha amani: Kobler

Picha: MONUSCO

Imani ya wananchi kwa UM ni muhimu ili kufanikisha amani: Kobler

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Martin Kobler ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa mkanganyiko wa amani na kukata tamaa miongoni mwa wananchi wa DRC unalazimu hatua mpya ili kurejesha imani yao kwa Umoja huo. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Kobler katika ripoti yake amesema tamasha la amani huko Goma, mwezi Septemba tarehe 21 lilileta matumaini ya amani lakini wiki mbili baadaye ,waasi wa ADF walisababisha mauaji jambo lililoibua hofu kwa wananchi na hata wengine kutaka kuvamia ofisi za MONUSCO.

(Sauti ya Kobler)

"Ni vitendo pekee dhidi ya ADF na sio maneno, ambavyo vitarejesha imani ya jamii kwa jeshi la DRC . na MONUSCO. Katika vita vyovyote hakuna ushindi unaopatikana bila ushirikiano wa jamii."  

Kobler pia amegusia kufukuzwa kwa afisa wa haki za binadamu huko DRC baada ya ripoti ya Likofi..

(Sauti ya Kobler)

"Kazi yetu ni shirikishi na ina malengo mazuri ya kuimarisha mamlaka ya kimaadili ya serikali.”

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Maziwa Makuu Said Djinnit akagusia suala la FDL kujisalimisha.

(Sauti ya Djinnit)