Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova.Picha/UM/Amanda Voisard

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO amelaani vikali tukio la kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Mexico Fuentes Rubio.

Katika taarifa yake Irina Bokova amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mauaji ya mwandishi huyo wa kike ambaye alikuwa mstari wa mbele kuwatetea wanyonge.

Amezitaka mamlaka kuanzisha uchunguzi wa haraka kujua mazingira ya mauaji hayo na kuisha wahusika wake kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.