Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyombo vya habari vimepuuza kuandika kuhusu athari za wahamiaji na usalama wa chakula-IFAD

Mkulima Cecilia Williams akiwa shambani picha@IFAD

Vyombo vya habari vimepuuza kuandika kuhusu athari za wahamiaji na usalama wa chakula-IFAD

Utafiti mmoja ulioratibiwa na shirika la maendeleo ya chakula IFAD umesema kuwa kwa asilimia kubwa taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari haziwagusi moja kwa moja waathirika wa uhamiaji.

Ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina la “yale yasiyoelezwa kuhusu chakula na uhamiaji” imesema kuwa kutowapa nafasi ya kujieleza kwa watu wanaotumbukia kwenye uhamiaji kumefanya mambo mengi yaendelee kufichika.

Mmoja wa wataalamu walioshiriki kuandaa ripoti hiyo Sam Dubberley amesema kuwa vyombo vingi vya habari vimepuuza kuandika habari kuhusu wahamiaji na tatizo la usalama wa chakula.

Baadhi ya wataalamu wamesema kuwa vyombo hivyo vinapuuza kuandika kuhusu wahamiaji hao kwa vile vinaona kwamba kuhama kwao hakuwezi kuathiri shughuli za kilimo kwa sababu idadi kubwa ni wakulima maskini wasiokuwa na tija katika uzalishaji wa chakula.