Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia iko njiapanda. Lazima tuchukue uamuzi thabiti: Obama

Rais Barack Obama wa Marekani akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Mark Garten)

Dunia iko njiapanda. Lazima tuchukue uamuzi thabiti: Obama

Rais Barack Obama wa Marekani amehutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akisema kikao hicho kinafanyika dunia ikiwa njiapanda ya mambo mengi ikiwemo amani au vurugu, kuungana au kutengana.

Amesema dunia inazidi kukumbwa na changamoto kuanzia za kiuchumi haki kijamii ikiwemo ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi na mizozo huko Syria na Iraq lakini kwa pamoja amesema dunia inaweza kuibuka mshindi.

Obama amesema mkutano huu ni fursa ya kufanya uamuzi thabiti.

(Sauti ya Obama)

"Tunakutana pamoja kama Umoja wa Mataifa, tunaweza kurejelea mfumo wa kimataifa uliowezesha maendelea makubwa au tunaweza kujiruhusu wenyewe kurudishwa nyuma na migogoro, au tunaweza kuthibitisha wajibu wetu wa pamoja wa kukabililiana na matatizo ya dunia hii, au tufunikwe na milipuko zaidi ya kukosekana kwa utulivu. Lakini leo napenda kuzingatia masuala mawili yenye kufafanua mizizi ya changamoto nyingi. Iwapo mataifa haya leo yanaweza wa kurejelea misingi ya kuanzishwa kwa umoja wa mataifa, au tutaungana kukataa kansa ya vikundi vyenye msimamo mkali"

Mapema akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewaeleza viongozi wa nchi na serikali kuwa mwaka huu umekumbwa na mambo mengi kuanzia ugaidi, watu kuuawa kwa kukatwa vichwa, njaa na mapigano akisema misingi ya Umoja huo imekumbwa na majaribu makubwa.