Ban akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ulaya

UN Photo.
Katibu mkuu Ban Ki-moon. Picha:

Ban akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ulaya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa kamisheni ya Ulaya José Manuel Barroso pamoja na rais wa baraza la Ulaya  Herman van Rompuy ambapo viongozi hao wamejadili hatua za dharura za kupambana na ugonjwa wa Ebola.

Viongozi hao kadhalika wamejaili mgogoro hususani nchini Ukraine  na madhara yake kwa nchi zinazopakana na nchi hiyo.

Katika hatua nyingine mkutano huo umeangazia pia umuhimu wa hatua za pamoja kuhusu atahri za mabadiliko ya tabianchi.