Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatuwezi kuzungumzia elimu bora kwa msichana bila kutathmini anavyotazamwa: Michelle

Hatuwezi kuzungumzia elimu bora kwa msichana bila kutathmini anavyotazamwa: Michelle

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa kutathmini mpango wa elimu kwanza duniani wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ambapo washiriki wameelezwa kuwa suala la elimu bora kwa wote litakuwa na mantiki zaidi iwapo ushiriki wa mtoto wa kike utatathmini kuanzia kwenye jamii yake na atapatiwa fursa kama ilivyo kwa wanaume.

Hoja hiyo iliwasilishwa na mmoja wa watoa mada Michelle Obama, Mke wa Rais wa Marekani ambaye alitolea mfano wake yeye mwenyewe akisema babu na baba yale walimthamini na kuwekeza kwake tangu alipozaliwa.

(Sauti ya Michelle)

“Wanaume ambao walinishikiza nifanikiwe shuleni, kwamba nini fursa sawa kama kama zangu, wakinisihi kuwa nipate mume ambaye ataishi nami akitambuwa kuwa sote tuko sawa. Suala la elimu ya sekondari kwa mtoto wa kike linanigusa pia mimi kama mama. Wengi wetu hapa ni wazazi au babu au bibi. Je nani atakubali mtoto wake wa kike apate tu elimu ya msingi?”

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson akaenda mbali zaidi akisema elimu bora ni zaidi ya tiketi ya kupata ajira na badala yake.

(Sauti ya Eliasson)

“Ni msingi wa mtu kuweza kukidhi mahitaji yake, usawa wa kijinsia, kutangamana kwenye jamii, maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi na uwajibikaji wa raia wa dunia.”

Mpango huo wa elimu kwanza duniani ulianzishwa mwaka 2012.