Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi ziweke wazi bajeti za jeshi-wito

UN Photo/Amanda Voisard
Alfred de Zayas, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya ukuzaji demokrasia na usawa wa utaratibu. Picha:

Nchi ziweke wazi bajeti za jeshi-wito

Mjumbe huru wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya ukuzaji demokrasia amesema kuwa kuna haja sasa kwa mataifa kuanza kuweka wazi bajeti inayotumika kugharimia vikosi vya kijeshi ili wananchi wapate fursa ya kuamua kipi kizingatiwe katika bajeti hizo.

Mjumbe huyo Alfred de Zayas amesema kuwa kuweka wazi matumizi hayo kutafungua njia kwa wananchi kuwa na usemi juu ya gharama zinazojitokeza na hivyo kutoa fursa kwa dhana ya uwazi na uwajibikaji kuonekana.

Amesema ni wakati muafaka kwa mataifa duniani kuanza kupunguza bajeti zake za kijeshi ili maeneo mengine kama elimu yapewe kipaumbele.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia, bajeti kwa ajili ya kugharimia jeshi inachukua kiasi cha asilimia 30 mpaka 40 ya bajeti nzima ya nchi.