Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yahaha kusaidia waaathirika wa mzozo Iraq

Mashirika ya UM yahaha kusaidia waaathirika wa mzozo Iraq

Licha ya kuendele kwa mzozo nchini Iraq kunakosababisha raia kukosa makazi, mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wa misaada ya kibinadamu yanahaha kuokoa maisha ya raia hao kutoka kusini mwa nchi katika eneo liitwalo Basra hadi jimboni Anbar, Duhok na Kurdistan.

Kwa mujibu wa mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Iraq Jacqueline Badcock, zaidi ya maeneo 1500 ya nchi hiyo yanahitaji misaada ya kibinadamu ya dharura na ulinzi kuweza kuishi katika mazingira hatarishi.

Ameongeza kuwa mashirika hayo yatasalia hapo kuhakikisha misaada ya usaidizi inawafikia walengwa katika maeneo yote nchini humo ambapo takribani watu milioni moja na laki nane hawana makazi.