Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN Women, FAO, na IFAD zazindua tuzo ya ubunifu wa sayansi kwa vijana

UN Women, FAO, na IFAD zazindua tuzo ya ubunifu wa sayansi kwa vijana

Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, yakiwemo la masuala ya wanawake, UN Women, lile la Chakula na Kilimo, FAO na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD, yametangaza tuzo mpya ya ubunifu wa kisayansi kwa vijana, ambayo itatolewa kwa wanafunzi binafsi au makundi ya wanafunzi.

Vijana wanaombwa kuwasilisha michanganuo ya ubunifu au teknolojia, ikiangazia ubunifu au teknolojia itakayowafaidi wanawake wakulima wa mashamba madogo, au ubunifu na teknolojia zinazofaidi watu wenye ulemavu wanaofanya ukulima wa mashamba madogo.

Michanganuo itazingatiwa kulingana na vigezo vifuatavyo

· Uimarishaji wa usalama wa chakula

· Uboreshaji wa lishe

· Kuongeza mapato na mazao

· Kuboresha na uzalishaji wa mapato

· Kupunguza kazi ya mikono na wakati mwingi unaohitajika kwa uzalishaji.

. Kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi

. Utumiaji wa rasilmali zinazopatikana kienyeji na kwa bei nafuu, na endelevu kijamii, na kupunguza upungufu baada ya mavuno.

Nchi zinazoshiriki ni Burundi, Djibouti, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Musumbiji, Rwanda, Somalia, Afrika Kusini, Sudan Kusini, Tanazania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Jinzi ya kuwasilisha:

Maelezo ya utaratibu wa kuwasilisha michanganuo yanapatikana kwa tovuti ya Sharefair: www.empowerwomen.org/ sharefair2014/ysia

Tuma fomu uliyoijaza kwa kwa:

youngscientistaward@sharefair2014.org Kabla au mnamo 15 Agosti 2014.

Tuzo zitakabidhiwa kwa kijana binafsi au makundi ya wanfunzi walioko katika shule au chuo pekee, na lazima thibitisho la kuwa mwanafunzi litolewe.

*Vijana wa kike wanahimizwa kutuma maombi yao*