Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti yataja mambo Makuu matano muhimu kwa maendeleo baada ya 2015

Ripoti yataja mambo Makuu matano muhimu kwa maendeleo baada ya 2015

Dira na wajibu wetu ni kutokomeza ufukara kwa minajili ya kuweka maendeleo endelevu na ustawi wa kudumu kwa wote, hiyo ni kauli tangulizi ya ripoti ya jopo la watu mashuhuri lililoundwa kutoa mapendekezo ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Jopo hilo la watu 27 likiongozwa na Rais Susilo Bambang Yudhoyono waIndonesia, Ellen Johnson Sirleaf waLiberiana Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron limetoa ripoti hiyo ya kurasa 81 ambayo inataka ajenda hiyo ya maendeleo izingatie mambo makuu matano. Mosi ajenda hiyo iwe jumuishi na mtu yeyote asiachwe nyuma kwa misingi yoyote ile ikiwemo jinsia, kabila, dini au rangi kwa kuwa maendeleo ya uchumi ni haki ya msingi ya binadamu. Pili inataka maendeleo endelevu iwe ndio msingi wa kila uamuzi, tatu chumi za nchi zifanyiwe mabadiliko makubwa ya kuwezesha ajira na ukuaji unaohusisha watu wote, nne ujenzi wa amani na taasisi wazi na wajibikaji na na mwisho ni kuwepo kwa ubia mpya wa kimataifa. Miongoni mwa wajumbe wa jopohilolililoundwa mwezi Julai mwaka jana na kufanya vikaoMonrovia, Bali,London na hapaNew York, ni John Podesta na hapa anaeleza kile walichoamini kitasukuma mbele maendeleo endelevu.

 (SAUTI YA JOHN PODESTA)

 “Tunavyoangalia malengo ya maendeleo ya milenia tunafahamu sasa kuwa maendeleo endelevu yanahitaji zaidi ya kuongeza kiwango cha pato la ndani la Taifa, bali uwepo wa taasisi thabiti na wajibikaji na tunajua kuwa ni lazima kwa makusudi kabisa kufikia jamii ambazo kihistoria zimekuwa zinatengwa kwa misingi ya kijiografia, jinsia, makundi na rangi na kwamba ni lazima kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”

 Katika kuandaa mapendekezoyao, jopohilolilikuwa na mashauriano na vikundi zaidi ya Elfu Tano vya kiraia kutoka nchi 121.