Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya demokrasia: Vijana wapewe kipaumbele

UN Photo.
Siku ya Demokrasia. Picha:

Siku ya kimataifa ya demokrasia: Vijana wapewe kipaumbele

Leo tarehe 15 Septemba ikiwa ni siku ya kimataifa ya demokrasia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema maadili ya umoja wa mataifa yanapata changamoto wakati dunia inakumbwa na ghasia na migogoro, akiongeza kwamba hali hiyo inaonyesha kwamba mahali ambapo jamii si jumusishi, serikali haziwajibiki, hakuna usalama wala usawa.

Katika ujumbe wake wa siku hii Ban amesema kila mtu anapaswa kuweka kipaumbele suala la kuwezesha watu ambao hawana kazi, matumaini na ambao wamekata tamaa.

Halikadhalika amesema jamii inapaswa kuwapatia kipaumbele vijana, kwani ni aslimia 20 ya idadi yote ya watu duniani.

Amesema licha ya changamoto wanazokumbana nazo, vijana wana fursa nyingi ya kutimiza ndoto zao na kuchangia katika kuimarisha demokrasia duniani.

Katika siku hii ya kimataifa ya demokrasia, Katibu Mkuu amewaomba vijana wote kuchangia katika kujenga demokrasia jumuishi duniani.