Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kulikuwa na watalii milioni 21 zaidi wa kimataifa miezi 6 ya kwanza 2015

Kulikuwa na watalii milioni 21 zaidi wa kimataifa miezi 6 ya kwanza 2015

Idadi ya watalii wa kimataifa iliongezeka kwa asilimia 4 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2015, kulingana na kipimo cha Shirika la Utalii Duniani, UNWTO.

Maeneo mbalimbali ya utalii duniani yalipokea watalii wa kimataifa wapatao milioni 538 kati ya Januari na Juni 2015, ikiwa ni nyongeza ya watu milioni 21, ikilinganishwa na wakati kama huo mwaka 2014.

Kwa mujibu wa UNWTO, kulikuwa na ongezeko la asilimia 5 Ulaya, Asia, Pasifiki na Mashariki ya Kati na asilimia 4 katika maeneo ya Amerika.

Takwimu haba kutoka Afrika zinaonyesha upungufu wa asilimia 6 wa idadi ywa watalii wanaowasili katika eneo hilo. Kikanda, maeneo ya Karibi na Oceania yalipokea watalii wengi zaidi, idadi ikiongezeka kwa asilimia 7.

Usalama bado ni suala kuzingatiwa, na kulingana na Katibu Mkuu wa UNWTO, Taleb Rifai, licha ya kuwepo misukosuko zaidi, takwimu zinaonyesha kuwa utalii umeendelea kunawiri katika miaka mitano iliyopita.