Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shindano la tuzo ya uvumbuzi wa kitamaduni lazinduliwa

Shindano la tuzo ya uvumbuzi wa kitamaduni lazinduliwa

Tuzo ya uvumbuzi unaoendeleza uiano baina ya tamaduni imezinduliwa leo na Jumuiya ya Ustaarabu katika Umoja wa Mataifa, UNAOC kwa ushirikiano na kampuni ya BMW.

Tuzo hiyo inatunukiwa kwa miradi bunifu na endelevu duniani, ambayo huendeleza mazungumzo na uelewano baina ya tamaduni mbali mbali, na hivyo kuchangia amani na maendeleo.

Mashirika kumi yenye uwezo wa kupanuka na kuenea yatashinda tuzo ya usaidizi wa kifedha na wa kimkakati. Washindi wa tuzo hiyo watatangazwa kwenye jukwaa la 7 la UNAOC.

Maombi ya kushiriki katika shindano hilo yanapaswa kuwasilishwa kufikia Septemba 30, 2015, na maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti: interculturalinnovation.org.