Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inasaidia familia zinazorejea kwa hiyari CAR:

IOM inasaidia familia zinazorejea kwa hiyari CAR:

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekubaliana na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, na washirika wengine wa misaada ya kibinadamu kuzisaidia kurejea kwa hiyari na kujiunga tena na jamii,  familia za wakimbizi wa ndani zilizokuwa kwenye kambi ya Mpoko iliyopo kwenye uwanja wa ndege wa Bangui.

Msemaji wa IOM Geneva, Leonard Doyle amesema mapema mwezi April serikali ya mpito ya CAR ilitangaza mipango ya kufunga kambi ya Mpoko ifikapo mwisho wa mwezi Juni mwaka huu.

Inakadiriwa kuna wakimbizi wa ndani 18,000 ambao sasa hivi wanaishi katika kambi hiyo kwa mujibu wa baraza la wakimbizi la Denmark (DRC).

Kwa mujibu wa tathimini ya kurejea iliyofanywa na baraza hilo kambini hapo asilimia 70 ya wakimbizi wa ndani wamekubali kurejea au kuhamishwa kutoka eneo hilo na kutaja wanakotaka kwenda.

Tangu kuzuka kwa machafuko CAR mwaka 2013 zaidi ya watu 900,000 walikuwa wakimbizi wa ndani nchi nzima , lakini sasa ni watu 167,000 wabo wametawanywa na hali hiyo.