Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pembe ya Afrika imepokea watu zaidi ya 14,000 wanaokimbia Yemen:IOM

Pembe ya Afrika imepokea watu zaidi ya 14,000 wanaokimbia Yemen:IOM

Watu zaidi wanakimbilia Pembe ya Afrika wakati machafuko yakiongezeka nchini Yemen. Hadi sasa jumla ya watu 14,529 wasalijiwa kuwasili Pembe ya Afrika limesema Shirika la Kimataifa la Wahamiaji.

IOM limeongeza kuwa watu 9,703 kati ya wote wamewasili Djibouti huku waliosalia 4,826 wamewasili Somalia. Wengi wa waliowasili Somalia wamefikia bandari ya Bossaso na Berbera lakini pia Puntland imesajili watu zaidi ya 3,000 tangu mwezi Machi, huku wale waliofikia Somaliland ni 1,550.