Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi zaidi wa Kenya warudishwa nyumbani kutoka Uganda

Wakimbizi zaidi wa Kenya warudishwa nyumbani kutoka Uganda

Nchini Uganda, msafara wa pili wa wakimbizi wa Kenya ambao wameishi nchini humo tangu wakimbie ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2008 umeanza safari asubuhi hii na wakimbizi 526.

James Onyango, afisa wa maswala ya jamii wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) kwenye kambi ya Kiryandongo amemwambia mwandishi wetu John Kibego ambaye alishuhudia msafara huo ukiondoka kwamba, wakimbizi hao wamefikisha idadi ya waliorudishwa nyumbani hadi 1,231 wakiwamo wale wa wiki jana.

Hao ni sehemu ya karibu wakimbizi 1,500 ambao wamekuwa wangali ukimbizini kati ya karibu 6,000 waliopokewa Uganda wakati ghasia zilifikia kilele.

Kesho tutakuletea makala kuhusu harakati nzima ya kuwarudisha nyumbani kwa hiari.