Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udongo wenye rotuba ni msingi wa uzalishaji wa chakula:FAO

Udongo wenye rotuba ni msingi wa uzalishaji wa chakula:FAO

Wiki ya kimataifa ya udongo imeanza kwa msisitizo wa udongo kwa ajili ya maendeleo.Kwa mujibu wa mkurugunzi wa shirika la kilimo na chakula FAO kitengo cha ardhi na maji Moujahed Achouri akizungumza katika ufunguzi wa wiki hiyo mjini Berlin Ujerumani amesema , udongo wenye rutuba ni msingi wa uzalishaji wa chakula na ndio suala litakalokuwa ajenda muhimu katika sera zinazohusiana na udongo.

Mkutano wa wiki ya udongo unawaleta pamoja washiriki 550 kutoka nchi 78 wanohusika na masuala ya udhibiti na maendeleo endelevu ya udongo Lomoudia Thiombiano ni naibu mwakilishi wa FAO kwa Afrika na mtaalamu wa udongo .

(SAUTI YA LOMOUDIA THIOMBIANO)

"Mataifa mengi ya Afrika yameibua njia za kisasa za kilimo na maendeleo vijijini, kikubwa ni kujiuliza ni vipi tunapaswa kulinda udongo kufuatia ongezeko la watu na ongezeko la mahitaji. Tunahitaji kilimo mseto na kusisitiza umuhimu wa usindikaji kilimo ili kupunguza athari kwa ajili ya vizazi vijavyo na pia kutoa elimu kwa  vijana na watoto ili wapate uelewa wa  udongo kwa ujumla na uwezekano wa kukabiliana na mahitaji yanayoibuka."

FAO imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa ya masauala ya udongo na watunga sera kushirikiana kupunguza mmomonyoko wa udongo na kurejesha ardhi ambayo imeathirika na mmomonyoko katika hali ya kawaida.