Aina mpya za uhalifu zahalalisha mateso, mtalaam wa UM aonya
Mjini Geneva, Uswisi, Mkuu wa Idara ya Mikataba ya Haki za Binadamu katika Ofisi ya Haki za Binadamu, Ibrahim Salama, amezindua mkutano wa 44 wa Kamati dhidi ya Mateso akisema mafanikio ya kamati hii yamekuwa mengi katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, lakini bado kazi ipo.
Miongoni mwa mafanikio hayo ni uelimishaji unaofanyika na maofisa wa Haki za binadamu kwenye nchini kama Fiji, Sudan Kusini na Guinea Bissau, na Mfuko maalum wa kusaidia wahanga wa mateso.
Hata hivyo, amesema:
“Kwa upande mmoja maana ya mateso imepanuka kupitia falsafa ya sheria ambayo imeongeza kizingiti cha ulinzi chini ya sheria za kitaifa na kimataifa. Watu wengi zaidi wanalindwa na waathirika zaidi wanapewa haki zao. Kwa upande mwingine, mateso yamezidi kuhalalishwa hasa katika mazingira ya mapambano dhidi ya ugaidi na kutokana na aina mpya ya uhalifu."