Skip to main content

Kongamano la 14 la Watu wa asili limeanza leo New York

Kongamano la 14 la Watu wa asili limeanza leo New York

Ni muziki wa asili ya Kirusi  uliochezwa katika ukumbi wa Baraza Kuu kwa ajili ya uzinduzi wa kongamano la 14 la Watu wa asili, lililoanza leo mjini New York. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Rais wa Baraza Kuu Sama Kutesa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson.

Katika maswala yatakiyozungumzwa kwenye mkutano huo wa 14, ni uhusiano kati ya haki za watu wa asili na ajenda ya maendeleo ya baada ya mwaka 2015.

Katika maandalizi ya kongamano hilo wawakilishi wa watu wa asili wamebaini maeneo sita ya kuzingatia yakiwa ni: umuhimu wa kukusanya takwimu mahususi kuhusu watu wa asili, umiliki wa ardhi na matumizi ya rasilimali, mkakati maalum katika sekta ya afya na elimu, haki ya kutendewa haki, uwakilishaji na ushirikishaji katika maswala ya uamuzi.